23 Novemba 2014 - 14:01
Makubaliano ya Nyuklia ya Iran bado magumu

Mazungumzo kuhusu nyuklia ya Iran bado yanakabiliwa na vikwazo vikubwa, kutokana na pande mbili kuwa mbali na masharti ya makubaliano hayo.

Mazungumzo kuhusu nyuklia ya Iran bado yanakabiliwa na vikwazo vikubwa, kutokana na pande mbili kuwa mbali na masharti ya makubaliano hayo.
waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema "Tunafanyakazi kwa nguvu na tunamatumaini tunapiga hatua, lakini tuna mianya mikubwa, bado tuna mianya mikubwa, ambayo tunaifanyia kazi kuiziba."
Kerry , ambaye siku ya Ijumaa aliahirisha safari yake mjini Paris ili kubakia mjini Vienna kwa mazungumzo hayo, amekutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif mchana jana Jumamosi, ukiwa mkutano wao wa nne katika siku tatu.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier , pia akiwa mjini Vienna , amesema hili ni mwisho wa juma la mwisho la mazungumzo, baada ya miezi kadhaa ya majadiliano, wakati "wa ukweli".
Kunatakiwa kupatikana makubaliano ya kihistoria ambapo Iran inazuia shughuli zake zinazobishaniwa za kinyuklia ili ipate afueni kubwa ya miaka kadhaa ya vikwazo vya kimataifa vya kiuchumi.
Makubaliano hayo yanaweza kufikisha mwisho mkwamo wa miaka kumi na mbili ambayo ulileta uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya vinu vya kinyuklia vya Iran.
Lakini Israel ilishindwa kushambulia vinu hivyo kwa kuhofia majibu ya Iran yangekuwa ni makubwa zaidi ya inavyotarajiwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amezungumza na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumamosi kwa simu na kumwambia kuwa: "Mwanya wa kufikia muafaka bado ni mkubwa mkubwa...Kwa sasa kunahitajika uamuzi wa kisiasa”.
Wajumbe wa majadiliano wa Jamhuri ya kiislamu Iran wamesifiwa na maafisa wa chini hiyo kwa kulinda na kuheshimu misingi ya nchi yao katika mazungumzo hayo."
Duru za mataifa ya Ulaya katika mazungumzo hayo zimesema , "hakuna hatua muhimu zilizopigwa" na " nafasi ya kupatikana makubaliano iko chini mno".
"Ili kupatikana makubaliano Wairani ni lazima kutoa maridhio katika hali ya juu," amesema.
Kwa upande wa pili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imeonyesha nia yake yakufukia makubaliano na imeuthibitishia ulimwengu kuwa haina nia ya kutengeneza nyuklia, ila imesisitiza kuwa haitakubaliana na mashart yeyote yatakayolenga kusimamisha miradi yake ya amani ya nyuklia,kwani ni haki yake na si kinyume na kanuni za kimataifa.
Marekani , Urusi , China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimekuwa zikifanya majadiliano na Iran tangu Februari mwaka huu kubadilisha makubaliano ya mpito yaliyofikiwa mwaka mmoja uliopita kuwa makubaliano ya kudumu ifikapo Novemba 24.
Makubaliano kama hayo yana lengo la kupunguza hofu kwamba Tehran inatengeneza silaha za kinyuklia chini ya kivuli cha shughuli za kiraia za kujipatia nishati.
Yafaa kuashiria kwamba Jamhuri ya kiislamu ya Iran imekuwa kwenye vikwazo kwa Zaidi ya miaka thelathini ambapo Marekani imezuia pesa za nchi hii na kupelekea uchumi wa nchi hii kushuka, jambo ambalo limepelekea uadui wa dhati kati ya nchi hizi mbili. Kwa upande mwingine Israel imekuwa ikihofia sana maendelea ya Iran kwani Iran imekuwa ikisaidia raia wasio jiweza wa Palestina ambao ni tishio la utawala wa Israel, hivyo kufikiwa makubaliano ya nyuklia kuna maanisha kuanza mwisho wa Israel.